BAADA ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuibua udhaifu wa kisheria ya kodi inayochangia migodi mikubwa kurejeshewa Sh trilioni 1.1 ambazo ni tozo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), migodi hiyo imejibu hoja hiyo na kusisitiza kuwa ina haki ya kurejeshwa kodi hiyo kwa kuwa inafanya mauzo ya bidhaa zao nje ya nchi.

Chama cha Wachimbaji Madini na Nishati (TCME) katika taarifa yake waliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari, kilisema kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Mwaka 2014, inaeleza kuwa wafanyabiashara ambao mauzo yao yote hufanyika kwa kuuza nje ya nchi, hukadiriwa VAT kwa kiwango cha sifuri, kwa sababu hiyo hustahili kurejeshewa kodi ya VAT ambayo huilipa kupitia manunuzi wanayofanya nchini.

TCME ilijitetea kuwa marejesho hayo yanafanyika kwa uhalali na yanafuata matakwa ya sheria ya VAT. “Ni muhimu ikaeleweka kampuni hizi bado zinalipa kodi ya VAT ambayo huwa hairejeshwi iwapo yatafanya manunuzi ya bidhaa ama huduma ambazo kisheria hastahili marejesho,” ilieleza taarifa yao. Ripoti ya CAG iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita ilifichua kuwa malipo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka kwenye migodi mikubwa minne ya dhahabu ya Geita, Bulyanhulu, Mara Kaskazini, Pangea na mmoja wa Almasi wa Williamson ilirejeshewa VAT yenye thamani ya Sh bilioni 1,144 kati ya mwaka 2012 mpaka 2016.

 

Call us:
(+255) 026-2782454
Address:
P.O.Box 1086, Chaungingi ST, Njombe, Tanzania.
Telephone: (+255) 026-2782454
E-mail: info@kingsfm.co.tz
Location      Contact Us