media

Shirika la wanaharakati nchini Afrika Kusini, Afriforum, limetangaza Jumatatu hii Agosti 2 nia yake ya kuwasilisha maombi yake mbele ya mahakama ya kutaka mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aondolewe kinga ya kidiplomasia iliyotolewa na serikali ya Afrika Kusini.

Grace Mugabe anashtumiwa kumshambulia Gabriella Engels mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

"Tutaomba mahakama kusema kwamba uamuzi wa wa kumpa mkewe rais `mugabe kinga ya kidiplomasia ni kinyume cha sheria kwa sababu, kulingana na sheria yetu, kinga ya kidiplomasia haiwezi kutumika katika kesi kubwa ya uhalifu na unyanyasaji" Kallie Kriel, kiongozi wa Afriforum ameliambia shirika la habari la AFP.

Grace Mugabe alirudi Zimbabwe licha ya kutafutwa na polisi Afrika Kusini.

Mapema siku ya Jumapili jioni vyombo vya habari nchini Zimbabwe vilisema mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe alirejea nyumbani kutoka Afrika kusini licha ya kukabiliwa na mashtaka ya kushambulia mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja Johannesburg.

 

Inaeleweka kwamba Grace Mugabe alisafiri pamoja na mumewe siku ya Jumapili asubuhi.

Wawili hao walikuwa wanahudhuria mkutano wa kikanda Afrika kusini.

Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye analaumu Bi Mugabe kwa kumgonga, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.

Call us:
(+255) 026-2782454
Address:
P.O.Box 1086, Chaungingi ST, Njombe, Tanzania.
Telephone: (+255) 026-2782454
E-mail: info@kingsfm.co.tz
Location      Contact Us