Public health

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wananchi kutoamini taarifa za upotoshaji zinazo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu chanjo nchini. Amesema hayo katika uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio jijini Dodoma. “Hatutakubali kuona watu wachache kwa maslahi yao wakiiweka Tanzania hatarini kwa ugonjwa wa Polio,Vyombo vya usalama wachukulieni hatua wale wote wanaosambaza taarifa za uzushi na kupotosha jamii kuhusu chanjo,chanjo hizi ni salama” amesema Aidha, amesema kampeni hiyo itakua ni ya siku nne na itafanyika kwenye vituo vya huduma za afya pamoja na kuwafuata watoto wenye umri chini ya miaka mitano baada ya kisa cha ugonjwa huo kuripotiwa nchi jirani ya Malawi, Jumla ya Watoto 10,295,316 wanatarajiwa kufikiwa kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa awamu hii ya pili ambapo awamu ya kwanza iliyofanyika katika mikoa ya Njombe, Mbeya, Ruvuma na Songwe waliwafikia watoto 1,138,949 kati ya 983,542 waliokusudiwa.

X